DRC YAKABILIANA NA JANGA KUBWA: VIFO VYA EBOLA VYAVUKA 5,000 MAAMBUKIZI YAKIONGEZEKA

DRC YAKABILIANA NA JANGA KUBWA: VIFO VYA EBOLA VYAVUKA 5,000 MAAMBUKIZI YAKIONGEZEKA

Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo imethibitisha kuwa ugonjwa wa Ebola aina ya Bundibugyo umeondoa maisha ya zaidi ya watu 5,000, jambo linaloonesha jinsi mlipuko huo unavyozidi kuwa mbaya.

Ripoti iliyotolewa Ijumaa na Jopo la Rais linaloshughulikia Ebola inaonyesha kuwa tangu kuanza kwa mlipuko huo, idadi ya wagonjwa waliothibitishwa imefikia 10,351, huku vifo vikiwa 5,026.

Sekta ya afya pia imeweka wazi uwepo wa maambukizi mapya 77 pamoja na vifo vingine 34 vilivyotokea hivi karibuni.Kulingana na taarifa hiyo, mkoa wa Ituri ndio ulioathirika zaidi, ukiwa na asilimia 71 ya visa vyote nchini na asilimia 36.4 ya maambukizi mapya yaliyotangazwa.

Hadi sasa, maambukizi ya ugonjwa huo yamegusa mikoa 8 kati ya mikoa 26 ya nchi hiyo.Wataalamu wa afya waliongeza kuwa wagonjwa 1,101 bado wako wodini wakipata matibabu, huku watu 2,788 wakiwa wamepata nafuu na kupona kabisa.

Hata hivyo, jitihada za kukabili janga hili zinakumbana na kizingiti kikubwa cha ukosefu wa amani katika maeneo ya mashariki mwa DRC.

Katika baadhi ya maeneo, wananchi wanaopinga kanuni za afya wamekuwa wakiwatishia na hata kuwashambulia wahudumu wanaopambana na ugonjwa huo.

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *