Makamu wa Rais, Dkt. Philip Mpango amemwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan katika mazishi ya aliyekuwa kiongozi wa Kanisa Katoliki Papa Francisko.
Sherehe za kumuaga zinafanyika katika viwanja vya Santa Pedro, Vatican.
Katika maadhimisho ya Misa hiyo, Dkt. Mpango ameambatana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mahmoud Thabit Kombo.
Viongozi kutoka mataifa mbalimbali wameshiriki ibada hiyo ya mazishi.
