DATA ZA MAAFISA 41,000 WA UHAMIAJI MAREKANI ZAVUJISHWA VIBAYA BAADA YA SHAMBULIO LA MITANDAO

DATA ZA MAAFISA 41,000 WA UHAMIAJI MAREKANI ZAVUJISHWA VIBAYA BAADA YA SHAMBULIO LA MITANDAO

Udukuzi mkubwa wa kimitandao umeipiga pigo Wizara ya Usalama wa Ndani ya Marekani (DHS), baada ya taarifa za siri za zaidi ya wafanyakazi 41,000 kuwekwa wazi kwenye mtandao wa intaneti.

Data hizo zilizovujishwa zinahusisha majina, namba za simu, anwani za ofisi, pamoja na majukumu ya maelfu ya maafisa wanaofanya kazi katika Idara ya Uhamiaji na Forodha (ICE) na Idara ya Ulinzi wa Mipaka (CBP). Hili ni shambulio la tatu la kiusalama kuikumba serikali ya Marekani katika wiki za hivi karibuni.

Kundi linalojiita Department of Peace ndilo lililofanya udukuzi huo na kunyakua taarifa hizo kutoka DHS. Baadaye, mtafiti wa usalama wa mitandao na mwanahabari Maia Crimew, kwa ushirikiano na mtandao wa Distributed Denial of Secrets, waliziweka taarifa hizo hadharani kupitia hifadhidata iliyopewa jina la Icepick.

Msemaji wa DHS ameeleza kuwa wizara hiyo inashughulikia kwa dharura mtafaruku huo wa kiusalama ili kulinda usalama wa maafisa wake, akisisitiza kuwa wanachukulia kwa uzito mkubwa kitisho chochote kinachoelekezwa kwa watumishi wa serikali.

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *