Waziri Mkuu wa Kanada Mark Carney amesema nchi yake iko tayari kuanza tena mazungumzo ya kibiashara na Marekani endapo Wamarekani watakuwa tayari.
Matamshi yake yanakuja baada ya Rais wa Marekani Donald Trump kutangaza kusitisha mara moja mazungumzo yote ya kibiashara na Canada kuhusu tangazo linalokosoa ushuru alioweka kwa taifa hilo.
Tangazo hilo, lililofadhiliwa na jimbo la Canada la Ontario, linamnukuu Rais wa zamani wa Marekani Ronald Reagan, Mrepublican na mwanahafidhina wa Marekani, akisema ushuru “unaumiza kila Mmarekani”
Trump aliandika kwenye mitandao ya kijamii kuwa tangazo hilo ni ‘feki’ na kuongeza kuwa mazungumzo ya kibiashara baina ya nchi hiyo yamefikia kikomo.

