Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wamepitisha bajeti ya shilingi trilioni 11. 783 ya Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) na taasisi zilizo chini yake zikiwemo Halmashauri.
Kwa mujibu wa Waziri wake, Mohamed Mchengerwa, bajeti hiyo imeongezeka kutoka shilingi trilioni 10.125 zilizotengwa mwaka 2024/25 hadi kufikia shilingi trilioni 11.783, ikiwa ni ongezeko la zaidi ya shilingi trilioni 1.66.

