Aziz Ki hati hati kuivaa Simba

Aziz Ki hati hati kuivaa Simba

Kiungo Aziz Ki ana aslimia 50 tu kuivaa Simba katika mechi ya watani wa jadi Machi 8,2025 kwa sababu ya maumivu ya nyonga.

Hili limesemwa na kocha wa Yanga Miloud Hamdi kuelekea mechi hiyo hapo kesho.

“Wachezaji wote wapo fiti kujiandaa na mchezo”,

“Mchezaji pekee ambaye nina wasiwasi nae ni Aziz Ki ambaye alipata shida ya mgongo,”

“Siwezi kusema kama atakuwepo au hatakuwepo bado ni 50/50 nafikiri mpaka kesho nitakuwa na majibu sahihi”

“Hii sio Derby yangu ya kwanza, nimewahi kucheza Derby ambayo ilikuwa na mashabiki tarkibani 120,000,”

” Siwezi kuwa na presha. Isipokuwa tu naheshimu wapinzani wangu, nasubiri tu mchezo mzuri na wa kuvutia,”

” Mashabiki waje kupata burudani wasiwe pia wasije na presha”, amesema kocha huyo.

“Ni matumaini yangu kuwa kesho tutafanya vizuri. Tumefanya maandalizi makubwa ya kutosha kuhimili presha ya Derby.

Kocha huyo ameongeza kuwa ;

“Hatuna wasiwasi na maandalizi yetu, kilichobaki ni kwenda kufanyia kazi kile ambacho tumeandaa kwenye uwanja wa mazoezi,”

“Tunaheshimu sana wapinzani wetu, lakini lazima ukweli uwekwe wazi kuwa sisi ni timu bora,”

“Natarajia kuona mchezo wa kimbinu sana, timu zote zina nguvu, timu zite zina dhamira ya kushinda mchezo unaokuja. Nadhani mchezo utakuwa wazi sana kwani kila timu inajiamini. Tunatarajia kuona mchezo ambao kila mtu atapambana kwa kila namna. Niseme tu sisi tupo tayari na tupo imara kwa mchezo huo” Miloud amesema.

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *