Kiungo Stephanie Aziz Ki amejumuishwa katika kikosi cha timu ya Taifa ya Burkina Faso.
Kocha Brama Traore wa timu hiyo amemjumuisha tena Stephane Aziz Ki katika kikosi cha Taifa hilo kitakachoingia kambini kujiandaa na mechi za kuwania kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Tunisia na Zimbabwe zitakazopigwa mapema mwezi Juni, 2025.
Aziz Ki aliyekuwa anakipiga Yanga amejiunga na Wydad Casablanca ya Morocco.

