Arsenal imemsajili kiungo mkabaji Martin Zubimendi kutoka Real Sociedad kwa mkataba wa muda mrefu, klabu hiyo ya Ligi ya Premia imesema.
Usajili huo ni katika kuimarisha eneo hilo kuelekea msimu ujao.
Hata hivyo, taarifa za kifedha kuhusu usajili huo hazikufichuliwa.
Lakini ripoti za vyombo vya habari vya Uingereza zilisema kijana huyo mwenye umri wa miaka 26 ana thamani ya kiasi cha euro milioni 60 ($70.67 milioni) wakati anatoka huko Sociedad ambapo alikuwa na kandarasi hadi 2027.
Zubimendi anakuwa mchezaji wa pili kusajiliwa na Arsenal katika kipindi cha karibu cha msimu huu baada ya kipa Kepa Arrizabalaga huku Mikel Arteta akipania kuimarisha kikosi ambacho kinaweza kuwa shindani kuwania ubingwa baada ya kumaliza washindi wa pili katika misimu mitatu iliyopita ya Ligi Kuu ya Uingereza.

