Ancelotti afurahishwa na ushindi wa Madrid

Ancelotti afurahishwa na ushindi wa Madrid

Meneja wa Real Madrid Carlo Ancelotti amesema kuwa alifurahishwa na ushindi wao wa 3-0 dhidi ya Valladolid licha ya timu yake kufanya vibaya wakati wa mechi hiyo ya LaLiga.

Licha ya kucheza vibaya mbali na kuwaanzisha wachezaji mahiri kama vile Kylian Mbappe, Vinicius Jr na Rodrygo, Ancelotti aliwamwagia sifa kemkem wachezaji wake wa akiba baada ya Brahim Diaz na Endrick kutoka kwenye benchi na kuihakikishia Real pointi kwa mabao ya dakika za lala salama baada ya Federico Valverde kutikisa nyavu dakika ya 50.

“Ladha ya ushindi huwa nzuri kila wakati, tunaposhinda mchezo lazima niwe na furaha, kwa kuzingatia ugumu tuliokuwa nao, haswa katika kipindi cha kwanza tulipokuwa polepole na laini,” Ancelotti aliambia mkutano na waandishi wa habari Jumapili.

“Tulikuwa bora baada ya mapumziko, tukiwa na uchezaji wa kasi zaidi katika kumiliki mpira,”

“Nina furaha sana wale wanaotokea benchi na kutumia dakika chache kupata ushindi,” amesema.

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *