Afisa Habari wa Klabu ya Yanga Ally Kamwe amesema hana taarifa kama amefungiwa na Shirikisho la soka nchini (TFF) kama inavyosambaa katika mitandao ya kijamii.
Fununu za Ali kufungiwa zimekuja baada ya yeye na msemaji mwenzake wa Simba Ahmed Ally kuhojiwa kwa kile kinachodaiwa kutoa maneno yasiyotakiwa katika michezo.
” Sijapokea taarifa rasmi ( barua) kuhusu suala hilo.
“ Sio mimi tu, hata klabu ya Yanga na wanasheria wanaoniwakilisha hawajapokea barua yoyote kuhusu hili,” amesema.
Ali Kamwe ameyasema hayo wakati alipokuwa akihojiwa na Kituo cha Redio cha Wasafi FM Machi 07, 2025 .
Kamwe amewataka wapenzi wa Yanga kutulia kusubiri taarifa rasmi.
“Ni kweli niliitwa na Kamati ya Maadili ya saa sabini na mbili ikiwa kesi yangu ya msingi nimeidhalilisha mamlaka kwa maana TFF na Bodi ya Ligi kwa kuzungumza maneno ya uongo yasiyokuwa na busara,” amesema Afisa Habari huyo wa Klabu ya Yanga

