Lewandowski: Tumewanyoosha Madrid

Lewandowski: Tumewanyoosha Madrid

Mshambulizi wa Barcelona Robert Lewandowski alifunga mabao mawili kipindi cha pili na kuwawezesha vinara Barcelona kuwalaza Real Madrid 4-0 katika ushindi wa kishindo wa Clasico kwenye LaLiga Jumamosi.

Mshambuliaji huyo wa Poland alipachika mabao mawili ndani ya dakika tatu mapema kipindi cha pili kabla ya Lamine Yamal mwenye umri wa miaka 17 kuwa mfungaji mdogo zaidi wa Clasico alipofunga dakika ya 77 na nahodha Raphinha kuhitimisha ushindi huo dakika sita kabla ya mchezo kumalizika.

” Ni ushindi wa kishindo na wa kihistoria katika kandanda la Uhispania na dunia kwa ujumla,” amesema.

Kwa ushindi huo, Barca wameendeleza uongozi wao kileleni waliposonga hadi pointi 30, sita juu ya Real na tisa mbele ya Villarreal katika nafasi ya tatu.

Baada ya vichapo vinne mfululizo vya Clasico, Wakatalunya hao walidai ushindi wao huo wa kwanza dhidi ya Real tangu Machi 2023 umewapa furaha iliyopitiliza.

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *