Kocha Juma Mgunda amekaribishwa Namungo baada ya kipigo cha 3-0 kutoka kwa mabosi wake wa zamani Simba katika mchezo wa Ligi Kuu katika uwanja wa KMC Mwenge.
Mgunda ameteuliwa kuwaoongoza wauaji hao wa Kusini ( Southern Killers) hivi karibuni.
Magoli ya Shomari Kapombe, Jean Ahoua na Fernanez Mavambo yaliiwezesha Simba ushindi huo muhimu.
Katika mechi nyingine usiku wa leo, Azam FC watapambana na KenGold.

