Shirika la Reli ( TRC) limetangaza kurejea kwa huduma baada ya ajali ya treni kutokea maeneo ya Ruvu mkoani Pwani.
Treni ya mwendo kasi imepata ajali leo Oktoba 23,2025 ambayo taarofa za awali inaelezwa kuwa ilitokana na hitilafu.
Treni hiyo ilikuwa ikisafiri kutoka Dar es Salaam kwenda Dodoma majira ya saa 2:00 asubuhi Oktoba 23, 2025.
Shirika limesema kuwa taarifa za awali hakuna tukio la kifo.
Imesema kuwa timu ya wataalamu inaendelea na uchunguzi wa kina na juhudi za kuhakikisha kwamba huduma zinarejea haraka.

