Alonso: Mbappe mguu sawa kuivaa Dortmund

Alonso: Mbappe mguu sawa kuivaa Dortmund

Kocha wa Real Madrid amesema kuwa Kylian Mbappe yuko tayari dhidi ya Dortmund katika katika mechi ya Robo Fainali ya kombe la Dunia la vilabu dhidi ya Dortmund.

Hata hivuo, kocha huyo Xabi Alonso alisema kuwa bado hakuna uhakika kama mshambuliaji huyo nyota ataanza katika mechi hiyo.

Mbappe alikosa mechi zote tatu za makundi kwenye michuano hiyo akiwa na tatizo la tumbo lakini akarejea kama mchezaji wa akiba wakati Madrid ilipoilaza Juventus 1-0 na kutinga hatua ya nane bora.

Hata hivyo, chipukizi Gonzalo Garcia ameiongoza Madrid katika michezo yote minne na kufunga mabao matatu nchini Marekani.

“Yeye ni bora, amekuwa akipata nafuu, tutaamua (kama ataanza),” Alonso aliwaambia waandishi wa habari Ijumaa.

Alisema Gonzalo anaweza kukipiga pamoja na Mbappe.

“Wanaweza (kucheza pamoja), kulingana na wakati na mahitaji” aliendelea Alonso.

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *