Aliyepinduliwa Mali apewa Urais wa ‘ mezani’

Aliyepinduliwa Mali apewa Urais wa ‘ mezani’

Kiongozi wa kijeshi wa Mali, Jenerali Assimi Goïta amepewa muhula wa urais wa miaka mitano na bunge la mpito na anaweza kuendelea tena kuongoza kwa kipindi kama hicho baadae bila kufanyika uchaguzi.

Kiongozi huyo wa kijeshi, ambaye amenyakua mamlaka mara mbili, aliahidi kurejea kwa demokrasia mwaka jana, lakini haikufanyika.

Mswada unaotoa mamlaka yake mapya ulisema unaweza kufanya hivyo “mara nyingi inavyohitajika hadi Mali itakapoka sawa.

Hatua hiyo inamfanya jenerali Goïta kuiongoza nchi hiyo ya Afrika Magharibi hadi 2030.

Hata hivyo, hatua hiyo imewafanya wengi kuhofia hatua hiyo inaweza kusababisha ukandamizaji wa upinzani.

Kiongozi huyo wa kijeshi mwenye umri wa miaka 41 aliteuliwa kuwa rais wa mpito baada ya mapinduzi yake mwaka 2021.

Wakati huo aliahidi kufanya uchaguzi mwaka unaofuata – lakini tangu wakati huo alikataa, kuwa pigo kwa juhudi za kurejesha utawala wa vyama vingi.

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *