Watu wawili wamefariki dunia katika mji wa Yokohama nchini Japan baada ya msichana kujirusha kutoka gorofani na kusababusha kifo kwa mpita njia.
Binti huyo aliyejirusha pia alimgonga mtembea kwa miguu na kusababisha kifo chake.
Mwanafunzi huyo wa shule mwenye umri wa miaka 17 aliruka kutoka kwenye jengo katika eneo la maduka lililojaa watu na kumgonga mwanamke mwenye umri wa miaka 32 ambaye alikuwa katika matembezi na marafiki zake Jumamosi jioni.
Wawili hao walipelekwa hospitali ambapo msichana huyo alifariki saa moja baadaye.
Mwanamke aliyemgonga pia alikufa muda mfupi karibuni.
Haijabainika kwa nini alijiua, ingawa watu wengi walio chini ya umri wa miaka 18 nchini Japani wanajiua ifikapo tarehe 1 Septemba – kabla tu ya muhula mpya wa shule kuanza , kwa mujibu wa takwimu rasmi.

