Takriban watu 330 wameuawa na mashambulizi ya anga ya Israel huko Gaza yaliyofanyika usiku kucha, kwa mujibu wa Wizara ya Afya inayoendeshwa na Hamas.
Jeshi la Israel limesema kuwa liliamua kufanya mashambulizi makubwa baada ya mazungumzo ya kuongeza muda wa kusitisha mapigano kushindwa kufikia makubaliano.
Ni wimbi kubwa zaidi la mashambulizi ya anga tangu Januari 19, wakati usitishaji mapigano ulipoanza kutekelezwa, anaripoti mwandishi wa BBC Gaza kutoka Cairo.
“Walifyatua moto wa mashambulizi tena ,” shahidi aliyeshuhudia katika Jiji la Gaza amesema.
Ofisi ya Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu imesema Israel “kuanzia sasa itachukua hatua dhidi ya Hamas kwa kuongeza nguvu za kijeshi”, ikishutumu Hamas kwa “kukataa mara kwa mara kuwaachilia mateka wao na kukataa mapendekezo ya kurefusha muda wa usitishaji mapigano.
Hamas inaishutumu Israel kwa kushambulia “raia wasio na ulinzi”, na inasema wapatanishi wanapaswa kuiwajibisha Israel kwa kukiuka na kupuuza usitishaji mapigano.

