MWIGULU NCHEMBA AMWAKILISHA RAIS SAMIA UFUNGUZI WA MKUTANO WA IPU ARUSHA

MWIGULU NCHEMBA AMWAKILISHA RAIS SAMIA UFUNGUZI WA MKUTANO WA IPU ARUSHA

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Nchemba, amemwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika hafla ya ufunguzi wa Mkutano wa 153 wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) ulioanza leo, Oktoba 5, 2026, jijini Arusha.Mkutano huo unafanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC) kuanzia Oktoba 5 hadi 9, 2026, ukiwakutanisha wabunge kutoka mataifa mbalimbali duniani.

Mkutano huo umebeba kaulimbiu inayolenga “Kuimarisha Utawala Bora na Kuwezesha Jamii kupitia Ushirikishwaji, Imani na Fursa kwa Wote,” ambapo washiriki wanajadili masuala mbalimbali yanayohusu utawala bora, demokrasia, maendeleo na changamoto zinazoikabili dunia.

Kwa Tanzania, mkutano huo ni fursa muhimu ya kuimarisha diplomasia ya kibunge, kubadilishana uzoefu na kujenga ushirikiano kati ya Bunge la Tanzania na mabunge ya nchi mbalimbali duniani.

Mkutano wa mwaka huu pia ni wa kihistoria kwa Tanzania kwa kuwa nchi imepewa nafasi ya kuandaa mkutano huo wa kimataifa, unaotarajiwa kuendelea hadi Oktoba 9, 2026.

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *