Shirikisho la Soka Afrika (CAF) limetoa orodha mpya ya vilabu bora 10 barani Afrika kuelekea msimu mpya 2024/25 wa mashindano ya vilabu barani Afrika huku klabu ya Simba ikiwemo katika orodha hiyo kutoka hapa Tanzania.
Vigogo wa Misri Al Ahly ambao ndio mabingwa wa kombe la mabingwa barani Afrika bado wanashikilia namba moja.
Kumekuwa na mabadiliko makubwa katika 10 bora, huku ES Tunis ikitoka katika nafasi ya tatu hadi ya pili, na kuipita Klabu ya Rulani Mokwena ya Wydad Athletic Club baada ya kufika fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Orodha kamili ni kama ifuatavyo:
- Al Ahly (Misri) – 87 points
- Esperance (Tunisia) – 61 points
- Wydad AC (Morocco) – 60 points
- Mamelodi Sundowns (Afrika Kusini) – 54 points
- Zamalek (Misri) – 48 points
- RS Berkane (Morocco) – 42 points
- Simba (Tanzania) – 39 points
- Petro de Luanda (Angola) – 39 points
- TP Mazembe (DR Congo) – 38 points
- CR Belouizdad (Algeria) – 36 points
Una maoni gani kuhusu orodha hii?

