Raia wa Guinea wanatazamiwa kupiga kura Jumapili katika Uchaguzi wao wa kwanza wa Urais tangu Mapinduzi ya Kijeshi miaka minne iliyopita. Kiongozi wa Kijeshi Mamadi Doumbouya anatarajiwa kushinda.
Wakosoaji wanasema kuwa Doumbouya amedhoofisha Upinzani tangu alipomtimua Rais wa zamani Alpha Conde, na hivyo kuacha ushindani mkubwa.
Wagombea tisa wanawania, lakini Mpinzani wake Mkuu ni Yero Balde wa Democratic Front ya Guinea.
Licha ya utajiri mkubwa wa Madini nchini Guinea, zaidi ya nusu ya watu wanakabiliwa na uhaba wa chakula, kulingana na mpango wa Chakula Duniani.
Takribani wapiga kura Milioni 6.7 wamesajiliwa, huku matokeo yakitarajiwa ndani ya saa 48 za Uchaguzi.

