Mchezo muhimu wenye tiketi ya Tanzania kufuzu WAFCON 2026, Twiga Stars dhidi ya Ethiopia utafanyika Azam Complex, Chamazi Jumatano hii saa 11 jioni.
Kwa mujibu wa Shirikisho la Soka nchini ( TFF), mechi hiyo haitakuwa na kiingilio ili kuipa hamasa ya ushindi timu hiyo ikiwa uwanja wa nyumbani.

