Kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo ( Chadema) Tundu Lissu inaendelea leo Julai 30, 2025 katika mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam.
Kesi hii inakuja ikiwa ni siku 14 tangu iliposikilizwa mara ya mwisho Julai 15, 2025.
Katika kesi iliyopita, Lissu wakatu anajitetea kuendelea kuahirishwa kwa kesi hiyo mara kwa mara na kuiomba Mahakama itumie mamlaka yake kufuta kesi hiyo kutokana na upande wa Jamhuri kuomba ahirisho mara kwa mara.
Ikumbukwe kuwa mara ya mwisho kesi hii kusikilizwa, Mahakama ilitoa uamuzi kwamba licha ya hoja za Lissu, Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Franco Kiswaga, aliutaka upande wa Jamhuri kuwa kama una nia ya kuendelea na kesi hiyo, basi hatua zichukuliwe kwa haraka ili shauri hilo liwasilishwe Mahakama Kuu.

