Mbwa ‘shujaa’ anayeokoa watu auawa kwa soseji

Mbwa ‘shujaa’ anayeokoa watu auawa kwa soseji

Mbwa “shujaa” wa kunusa ameuawa kwa soseji zilizojazwa misumari – huku waziri mkuu wa Italia akilaani kitendo hicho.

Mbwa huyo anayeitwa Bruno alifariki kutokana na kuvuja damu ndani baada ya chakula kutupwa kwa makusudi kwenye banda lake katika mji wa kusini wa Tarananto, kulingana na mkufunzi wake.

Arcangelo Caressa alisema mnyama huyo ambaye ameokoa binadamu wengi kifo chake ni cha uchungu – na akaonya kwa anayedaiwa kufanya kitendo hicho kwa kuandika kwenye Facebook “Ninajua wewe ni nani, na utalipia.”

Alisema Bruno daima atakuwa shujaa.

“Ulipigania maisha yako yote ili kumsaidia mwanadamu, na mwanadamu huyo huyo leo anakufanyi hivi,” Bwana Caressa aliongeza.

Bruno alifanikiwa kuwaokoa watu tisa, wakiwemo watoto waliopotea , vyombo vya habari vya Italia viliripoti.

Waziri Mkuu Giorgia Meloni alichapisha picha yake akimpa mbwa huyo tuzo, akiandika: “Habari ya kuhuzunisha. Kitendo kibaya, cha woga, kisichokubalika.

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *