Rais wa zamani wa Liberia William Tolbert anatazamiwa kuzikwa upya siku ya Jumanne, miaka 45 baada ya kuuawa wakati wa mapinduzi na mwili wake unaoaminika kutupwa kwenye kaburi la pamoja.
Siku kumi baada ya kuuawa kwa rais, kufuatia kesi za mahakama ya kangaroo, viongozi 13 wa baraza lake la mawaziri walivuliwa nguo, wakafungwa kwenye vigingi na kisha kuuawa kwa kupigwa risasi kwenye ufuo karibu na kambi ya jeshi katika mji mkuu, Monrovia.
Hakuna maiti yoyote kati ya 14 iliyopatikana lakini kila mmoja wao anatazamiwa kupata mazishi ya serikali katika hafla iliyohudhuriwa na Rais Joseph Boakai na viongozi wengine.
Mapinduzi ya tarehe 12 Aprili 1980 ambapo Sgt Samuel Doe akiwa mwenye umri wa miaka 28 alichukua mamlaka yalimaliza zaidi ya karne moja ya utawala wa kisiasa na Waamerico-Liberians wachache weusi walioachiwa huru ambao walikuwa wametoka Marekani katika miaka ya 1800.
Urais wa miaka tisa wa Tolbert ulidaiwa kuwa na ukosefu wa usawa wa kikabila.
Kupinduliwa kwake kulikuja mwanzoni mwa kipindi cha kukosekana kwa utulivu nchini Libeŕia, na kufikia kilele cha vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyosababisha maafa, ambavyo hatimaye vilimalizika mwaka 2003.
Doe mwenyewe alikumbana na kifo cha kikatili mikononi mwa waasi mwaka 1990.
Mazishi yake tena katika mji alikozaliwa wiki iliyopita pia yaliamriwa na rais.

