Rais Samia akemea wanaharakati kutoka nje kuingilia mambo ya ndani

Rais Samia akemea wanaharakati kutoka nje kuingilia mambo ya ndani

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amekemea wanaharakati wa kisiasa kutoka nje ya nchi wanaojaribu kuingilia mambo ya ndani ya Tanzania na kutaka kuivuruga amani.

Amevitaka vyombo vya ulinzi na usalama kukabiliana na wale aliosema wanajaribu kuchafua taifa hili baada ya kuharibu huko kwao.

Amesema inawezekana malengo ya wanaharakati hao ni kuvuruga amani ya nchi iliyojengwa kwa muda mrefu.

Rais Samia ameitoa kauli hiyo wakati akizindua sera ya mambo ya nje.

Kauli hiyo inakuja saa chache baada ya baadhi ya wanaharakati kutoka Kenya akiwemo Martha Karua kutoruhusiwa kuhudhuria kesi inayomkabili Mwenyekiti wa Taifa wa CHADEMA Tundu Lissu.

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *