Beki wa Liverpool, Virgil van Dijk amesaini mkataba mpya na timu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu ya Uingereza.
Beki huyo wa kati wa Uholanzi mwenye miaka 33, ambaye mkataba wake wa sasa unamalizika msimu huu wa joto, amesaini hadi 2027, klabu hiyo ilisema Alhamisi.
Hatua hii inakuja chini ya wiki moja baada ya nyota mwingine wa Liverpool, Mohamed Salah, kuongeza muda wake wa kukaa Anfield na ilikuwa miezi michache kabla ya mkataba wake kumalizika.

