Vikosi vya usalama vya Somalia vimefanikiwa kuzuia uvamizi wa wapiganaji wa Kiislamu ambao walivamia hoteli maarufu katikati mwa jiji la Beledweyne, mamlaka ilisema.
Mashambulizi ya al-Shabab yalianza kwa mlipuko wa bomu lililotegwa ndani ya gari, na kufuatiwa na watu wenye silaha walioingia ndani ya hoteli hiyo, na kusababisha makabiliano makali na vikosi vya usalama.
“Washambuliaji wamepunguzwa nguvu. Wengine walijilipua huku wengine wakiuawa na vikosi vya polisi,” Omar Osman Calasow, meya wa wilaya ya Beledweyne, aliambia BBC.
Meya huyo alisema watu saba wameuawa katika shambulizi hilo lakini walioshuhudia walisema idadi ya waliofariki inaweza kuwa kubwa zaidi.

